Washukiwa wawili wa ugaidi wakamatwa Mjini Mombasa

Washukiwa wawili wa ugaidiĀ  wamekamatwa na kitengo maalum cha maafisa wa upelelezi na wale wa kitengo cha kukabiliana na ugaidi mjini Mombasa Mombasa Jumatatu.

Also Read
Mshukiwa wa ugaidi akamatwa akipiga picha Kituo cha Polisi cha Makongeni

Washukiwa hao walikamatwa katika kivukio cha Feri cha Likoni upande wa bara baada ya maafisa wa upelelezi kufungia barabara na kuzingira gari aina ya Probox yenye nambari ya usajili KCE 695U kabla ya kuwakamata washukiwa hao wawili.

Also Read
DCI yatoa orodha ya washukiwa wanane wa ugaidi wanaosakwa

Bunduki mbili aina za AK-47, rununu,risasi na vifaa vingine vilinaswa wakati wa oparesheni hiyo ya pamoja.

Also Read
Shamra shamra zanoga huku siku kuu ya Eid ikikaribia

Kamanda wa polisi katika eneo la Pwani Manase Musyoka alisema uchunguzi umeanzishwa kuhusu kisa hicho.

  

Latest posts

Ngirici aondoa kesi mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Waiguru

Tom Mathinji

Rais Museveni awaomba Wakenya msamaha

Tom Mathinji

Joyciline Jepkosgei apandishwa cheo hadi Sergeant baada ya ufanisi wa London Marathon

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi