Washukiwa wawili wanaswa wakisafirisha Misandali ya thamani ya shilingi milioni 12

Maafisa wa polisi na wale wa huduma ya kitaifa ya misitu-KFS waliwatia mbaroni washukiwa wawili waliopatikana wakisafirisha tani tatu za miti aina ya Misandali.

Miti hiyo  ya thamani ya shilingi milioni 12 ilikuwa ikisafirishwa kupitia barabara kuu ya Isiolo-Marsabit.

Also Read
Serikali yatoa shilingi bilioni mbili kukabiliana na Ukame

Washukiwa walikamatwa baada ya maafisa kutoka kituo cha polisi cha Maralal kudokezwa na umma kwamba kulikuwa na lori moja lililokuwa limebeba shehena ya misandali katika msitu huko  Samburu mashariki.

Also Read
Mtu mmoja auawa na fisi, watatu wajeruhiwa huko Samburu

Dereva wa lori hilo alinaswa na polisi wa kituo cha Eldonyiro,kaunti ya Samburu  alipokuwa akijaribu kutoroka.

Maafisa hao wamewataka wakazi wa Samburu kutokata miti ya kiasilia kwenye msitu huo na kuwaripoti watakaotenda uhalifu huo kwa polisi katika juhudi za kutunza mazingira. Washukiwa hao wawili watafikishwa mahakamani Jumanne.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi