Wasi wasi Laikipia kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19

Serikali ya Kaunti ya Laikipia imeashiria kwamba itatangaza masharti zaidi ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.

Hii ni kufuatia kuongezeka kwa visa vya maambukizi mapya ya virusi hivyo katika kaunti hiyo.

Also Read
Kenya yatajwa kivutio bora zaidi cha watalii duniani mwaka 2020

Afisa Mkuu wa Huduma za Afya katika kaunti hiyo Dkt. Joseph Lenai Kamario amesema hali ya wasiwasi imeghubika kaunti hiyo kufuatia kuongezeka kwa maambukizi katika siku kadhaa zilizopita.

Also Read
William Ruto na Gideon Moi wahubiri amani katika mazishi ya Hosea Kiplagat

Kwa sasa Dkt. Kamairo amewahimiza wakazi kuchukua jukumu la binafsi kwa kuzingatia kanuni za kujikinga.

Amesema Idara ya Afya katika kaunti hiyo imepima jumla ya sampuli 6,703 tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha ugonjwa huo hapa nchini mwezi Machi mwaka huu.

Also Read
Watu 277 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Hadi sasa watu 410 wamebainishwa kuambukizwa korona katika kaunti hiyo, idadi inayowakilisha kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.12.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi