Wasimamizi wa Uchaguzi Katika Kiwango cha Maeneo Bunge Wagawa Vifaa Vya Kupigia Kura Hadi Vituo Vya Kupigia Kura

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu katika viwango vya maeneo bunge hivi leo wanagawa vifaa vya kupigia kura leo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura zikiwa zimesalia saa chache kabla ya shughuli ya kupiga kura kuanza. Kufikia jana jioni, wasimamizi hao walikuwa wamepanga vifaa hivyo ambavyo ni sanduku za kupigia kura, mihuri, spika, taa ya gesi kati ya vingine na karatasi za kupigia kura zilifunguliwa leo asubuhi mbele ya wasimamizi hao wa vituo vya kupigia kura.

Also Read
Maxine Wahome aweka historia ya WRC Safari Rally

Katika maeneo mengi shughuli hiyo inaendelea kwa njia sawa lakini katika maeneo machache kumetokea mkanganyiko. Zoezi hilo lilisimamishwa kwa muda katika eneo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa baada sanduku lililotarajiwa kuwa na makaratasi ya kupigia kura wadhifa wa ugavana kubainika kuwa na nembo ya kaunti ya Kilifi badala ya nembo ya kaunti ya Mombasa na ilipofunguliwa pia ilibainika kwamba makaratasi hayo yana orodha ya majina na picha za wawaniaji ugavana wa kaunti ya Kilifi badala ya wale wa kaunti ya Mombasa.

Also Read
Karauri awania ubunge Kasarani akidhamiria kuwainua kiuchumi wakaazi

Ulinzi pia ni jambo muhimu katika vituo vya kujumlisha kura katika maeneo bunge ambavyo vinatumika kugawa vifaa vya uchaguzi. Mwanahabari wa KBC Alvin Kaunda ambaye anaripoti kutoka eneo bunge la Kasarani kaunti ya Nairobi anaarifu kwamba alipitia msako mkali kabla ya kuingia kwenye kituo cha kujumlisha kura cha eneo hilo katika uwanja wa michezo wa Kasarani. Akiwa pale alizungumza na msimamizi wa kituo Bwana Amos Nyongesa ambaye alimwelezea utayari wao kwa shuguli ya kesho.

  

Latest posts

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

NMS yakabidhi majukumu yake kwa kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi