Wataalam wa WHO wawasili Wuhan kuchunguza chanzo cha Covid-19

Jopo la wataalamu wa shirika la afya duniani-WHO limewasili mjini Wuhan nchini China kuchunguza chanzo cha chamuko la virusi vya Korona.

Uchunguzi huo uliosubiriwa kwa hamu umeanza baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa kati ya shirika la WHO na serikali ya China.

Kundi hilo la wataalamu kumi linatarajiwa kuwahoji watu kutoka taasisi za utafiti, hospitali na masoko ya vyakula vinavyotokana na viumbe wa majini ambavyo vimehusishwa na chamuko la virusi vya Korona mjini Wuhan mwaka-2019.

Also Read
Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Kuwasili kwa kundi hilo kumejiri wakati ambapo visa vya maambukizi ya Korona vinaongezeka Kaskazini mwa China huku hali ya kawaida ikishuhudiwa jijini Wuhan.

Also Read
Maseneta wa Marekani wapitisha mswada wa dola trilioni 1.9 za kukabiliana na athari za korona

Wanasayansi hao watajitenga kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuanza shughuli hiyo ambayo itategemea pakubwa sampuli na ushahidi kutoka kwa maafisa wa serikali ya taifa hilo.

Uchunguzi huo unaolenga kubaini fununu kwamba virusi vya korona vilitokana na mnyama ulikumbwa na sintofahamu ila kwa sasa kila kitu kiko tayari kwa zoezi hilo.

Also Read
Rwanda yathibitisha kuwepo aina mpya ya Covid-19 nchini humo

Mapema mwezi huu shirika la WHO lilisema maafisa wake walizuiliwa kuingia nchini China baada ya mmoja wa maafisa hao kuzuiliwa kuingia nchini humo na mwingine akikwama kwenye safari akielekea nchini humo.

  

Latest posts

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi