Watafiti wa humu nchini wajizatiti kutafuta tiba ya kuumwa na nyoka

Kituo cha kitaifa cha utafiti na matibabu kuhusu sumu ya nyoka kimeanzisha utafiti kuhusu nyoka wenye sumu kali katika kaunti ya Baringo.

Lengo la utafiti huo ni kupambana na uhaba ulioko wa dawa za kutibu visa vya kuumwa na nyoka humu nchini.

Also Read
Shule kadhaa Baringo huenda zisifunguliwe kesho kwa hofu ya mashambulizi

Mnamo miezi ya hivi punde kumekuwa na ongezeko la visa vya watu kuumwa na nyoka kwenye kaunti za Baringo, Kitui na pia baadhi ya maeneo ya pwani.

Mkuu wa mpango wa kitaifa wa utafiti na matibabu kuhusu sumu ya nyoka Dkt. George Omondi anasema utafiti huo utawezesha Kenya kupambana na uhaba ulioko wa dawa za kutibu visa vya kuumwa na nyoka.

Also Read
Watahiniwa wa KCPE na KCSE katika kaunti ya Baringo wahakikishiwa usalama wao

Alisema kituo hicho kimekuwa kikitumia mbinu zisizo za kutegemewa katika kutibu kuumwa na nyoka  nchini Kenya.

Katibu katika wizara ya wanyapori Prof. Fred Segor alisema wizara hiyo itaunga mkono utafiti huo sawia na upatikananji wa dawa za kutibu kuumwa na nyoka katika kanda hii.

Also Read
Mgomo wa kitaifa wa madaktari kuanza Jumatatu

Aidha, kituo hicho kinatumai kuhusisha  jamii zaidi, jambo ambalo limetambuliwa kuwa muhimu katika kupunguza visa vya kuumwa na nyoka kufikia mwaka 2030.

  

Latest posts

Kithure Kindiki ajiondoa katika ulingo wa kisiasa

Tom Mathinji

Raila Odinga atangaza sehemu ya baraza lake la Mawaziri

Tom Mathinji

Kalonzo Musyoka asema kwaheri kwa Muungano wa Azimio la Umoja

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi