Watalii kuingia Mbuga ya Kitaifa ya Ziwa Nakuru kupitia viingilio vya Lanet na Nderit

Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori nchini, KWS, limesema kuwa wageni wanaweza kuingia kwenye Mbuga ya Kitaifa ya Ziwa Nakuru kupitia viingilio vya Lanet na Nderit baada ya kiingilio kikuu kusombwa na maji.

Mlinzi Mkuu Collins Ochieng amekanusha ripoti kwamba hifadhi hiyo maarufu duniani ya ndege na wanyama pori imefungwa baada ya viwango vya maji kwenye Ziwa Nakuru kuongezeka kupita kiasi na kuharibu majengo na barabara kwenye mbuga hiyo.

Also Read
Mama Taifa ampongeza Jim Nyamu kwa juhudi zake za kuwatunza Ndovu

Alisema hayo kwenye afisi za shirika la KWS katika mbuga hiyo mwishoni mwa wiki baada ya kushauriana na msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna, kamishna wa kaunti Erastus Mbui Mwenda na Naibu Gavana Dkt. Eric Korir kuhusiana na athari za ongezeko hilo la viwango vya maji kwa mfumo ikolojia wa ziwa hilo.

Also Read
Serikali yajizatiti kuimarisha mifumo ya usafiri na uchukuzi kote nchini

Alisema kuwa shirika hilo limetumia kiasi cha shilingi milioni 38 kukarabati muundo msingi katika mbuga hiyo.

Oguna kwa upande wake amesema kuwa Waziri wa Utalii Najib Balala mnamo mwezi Julai mwaka huu alipunguza kwa nusu ada za kiingilio za Wakenya kwenye mbuga na hifadhi katika juhudi za kuwavutia watalii zaidi wa humu nchini.

Also Read
Machakos yanakili visa 1,300 vya Covid-19 tangu virusi hivyo kuripotiwa humu nchini

Alisema kuwa Wizara ya Utalii imesitisha kwa mwaka mmoja ulipaji kodi kwa hoteli zinazotekeleza huduma zao ndani ya mbuga na kwenye maeneo mengine ya kitalii.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi