Watu watatu wameangamia baada ya mashua kupinduka na kuzama kwenye Ziwa Baringo.
Akithibitisha mkasa huo, Kamanda wa Polisi katika Kaunti Ndogo ya Baringo Kusini Benjolliffe Munuve alisema mashua hyi ilikuwa na abiria wengi kupita kiwango chake.
Munuve amesema mashua hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria wanane ilikuwa imebeba abiria 12 na ilikuwa ikisafiri kutoka Kampi Samaki, ilipozama majini ilipokuwa ikielekea kisiwa maarufu cha Kokwa.
Iliarifiwa kuwa wanne kati ya abiria hao waliogelea na kujinusuru.
Mashua hiyo ilikuwa ikisafirisha familia mbili zinazoishi kwenye Kisiwa cha Kampi Samaki.
Wengine tisa waliokolewa, huku watatu, akiwemo mhudumu wa mashua hiyo, na mtoto wa umri wa mwaka mmoja na vile vile msichana wa umri wa miaka 16 wakizama kwenye mashua hiyo.