Watoto wawili wauawa na Kiboko ufuoni Ziwa Victoria

Watoto wawili wamefariki baada ya kushambuliwa na Kiboko katika maeneo ya Siungu na Uhwaya kwenye fuo za Ziwa Victoria, Kaunti Ndogo ya Bondo.

Katibu wa kikundi cha usimamizi wa eneo la ufuo la Siungu, Erick Ochieng, amesema watoto hao walikuwa wakioga katika eneo hilo la ufuo wakati waliposhambuliwa na Kiboko.

Also Read
Idadi ya watalii wanaozuru mbuga ya Hells gate yaongezeka

Ochieng amesema mnyama huyo alimshambulia mtoto wa kwanza mvulana, ambaye alikuwa wa gredi ya kwanza, katika ufuo wa Siungu kabla ya kuelekea eneo jingine la ufuo wa Uhwaya ambako pia alimshambulia na kumjeruhi vibaya mvulana mmoja wa darasa la nane, ambaye anaendelea kutibiwa katika hospitali moja ya sehemu hiyo.

Also Read
NTSA yasimamisha shughuli za magari ya uchukuzi ya chama cha KISTAG

Amesema mtoto wa tatu ambaye aliumwa tumboni na mnyama huyo huyo, alitangazwa kuwa amefariki baada ya kufikishwa kwenye kituo cha afya cha Got Agulu.

Also Read
Utovu wa Usalama watatiza masomo Laikipia Magharibi

Wavuvi katika eneo hilo wametoa wito kwa serikali kuingilia kati kupitia kwa Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori nchini (KWS), ili kuhakikisha mnyama huyo amenaswa ama kuhamishwa katika juhudi za kukomesha mizozo kati ya wanadamu na wanyama katika eneo hilo.

  

Latest posts

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Watu watano wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wakili Willie Kimani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi