Maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 nchini yanaendelea kuongezeka na kutimia asili mia 29.6, huku watu 1,020 zaidi wakithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo baada ya sampuli 3,444 kupimwa katika muda saa 24 zilizopita na kufikisha idadi jumla ya watu 264,727 walioaambukizwa ugonjwa huo hapa nchini, baada ya sampuli milioni 2.9 kupimwa.
Kati ya idadi hiyo mpya watu 906 ni raia wa Kenya na 114 wakiwa raia wa kigeni, huku 534 wakiwa wanaume na 486 wanawake. Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa mwaka mmoja na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 95.
Wagonjwa wengine 19 wamepona ugonjwa huo, 14 kutoka vituo mbali mbali vya afya kote nchini na watano kutoka mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani.
Hakuna aliyeripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo katika muda wa saa 24 ziolizopia na idadi ya waliofariki imesalia kuwa 5,353.
Takriban wagonjwa 288 wamelazwa katika taasisi tofauti za matibabu huku wengine 5,631 wakiendelea kushughulikiwa nyumbani.
Jumla ya watu 249,315 wamepona ugonjwa huo hapa nchini, 201,154 kutoka mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani na 48,161 walitoka katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini.
Wagonjwa 16 zaidi wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, tisa kati yao wanatumia mitambo ya kuwasaidia kupumua na saba wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen.
Hadi kufika tarehe 19 mwezi Disemba mwaka 2021, jumla ya watu 8,902,539 walikuwa wamechanjwa dhidi ya Covid-19 kote nchini. Kati ya watu wao 5,310,496 wamechanjwa awamu ya kwanza na 3,592,043.