Watu 179 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kenya imenakili visa 179 zaidi vya virusi vya covid-19 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idaidi hiyo iliafikiwa baada ya kupimwa kwa sampuli 4,423.Hii inafikisha idadi jumla ya visa vilivyothibitishwa nchini kuwa 102,792.

Kati ya maambukizi hayo mapya, watu 151 walikuwa wakenya huku 28 wakiwa raia wa kigeni.

Also Read
EPRA: Bei za mafuta kusalia jinsi zilivyo

Watu 87 walikuwa wanawake huku 92 wakiwa wanaume.

Mgonjwa mchanga zaidi alikuwa mtoto wa mwezi mmoja huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 93.

Also Read
Watu 123 wathibitishwa kuambukizwa COVID-19, huku wagonjwa 412 wakipona

Kaunti ya Nairobi ingali kuongoza kwa visa 127 huku ikifuatwa na kaunti ya Nandi kwa visa 11 na kaunti ya Mombasa kwa visa saba.

Mgonjwa mmoja alifariki na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kuwa 1,795.

Also Read
IEBC yachapisha rasmi majina ya washindi wa chaguzi ndogo za hivi punde

Wagonjwa 79 walipata nafuu huku 62 wakiwa wale waliokuwa wakitibiwa nyumbani na 17 wakitoka katika hospitali mbalimbali nchini.

Idadi jumla ya waliopata nafuu sasa ni watu 84,952.

Kwa sasa wagonjwa 345 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi