Watu 20 wakamatwa Samburu kufuatia msako wa kuhimiza kanuni za COVID-19

Watu 20 wamekamatwa baada ya kupatikana wakinywa pombe kwenye nyumba za kukodisha Jumapili usiku mjini Maralal katika kaunti ya Samburu.

Naibu wa Chifu mjini Maralal Celina Lemakara aliwaongoza maafisa wa polisi, wazee wa kijiji na nyumba kumi kwenye msako huo.

Also Read
Magoha azuia maafisa wa NYS kusimamia KCSE

Watu kadhaa miongoni mwao wanafunzi walikamatwa kwenye baa, maeneo ya unywaji pombe na nyumba za makazi.

Lemakara aliwaonya wenye baa dhidi ya kuuza pombe baada ya saa tatu usiku.

Amesema kuwa baadhi ya wafanyibiashara wanaomiliki biashara za mvinyo wanauza bidhaa hiyo kwa watu ambao wamegeuza nyumba za makazi kuwa maeneo ya unywaji pombe.

Also Read
Kongamano kuhusu Ugatuzi kuendelea jinsi ilivyoratibishwa

“Nimeshika watu 20 hapa na wengine ni wanafunzi. Kwa hivyo mimi naomba wazazi, machifu wenzangu na maafisa wote wa usalama tuendelee kufanya misako mpaka mji huu unyoroke,” amesema Lemakara.

Also Read
Echesa kusalia korokoroni akisubiri uamuzi wa iwapo atazuiliwa kwa siku saba zaidi

Aidha, Lemakara amewataka wazazi kuwachunga watoto wao akisema kuwa miongoni mwa wale waliokamatwa ni wanafunzi wanaotarajiwa kurejea shuleni mwezi Januari mwaka ujao ukiwa umesalia muda wa mwezi mmoja pekee.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi