Watu 20 wauawa na wanamgambo katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo

Takribani watu 20 waliuawa mwishoni mwa Juma kwenye mashambulizi ya wavamizi walioshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu mashariki mwa Jamhuri ya ki-demokrasia ya Congo.

Hayo ni kwa mujibu wa habari zilizotolewa na jeshi, na pia shirika moja la kutetea haki za kibinadamu nchini humo.

Also Read
Washukiwa watano wa ugaidi wauawa nchini Uganda

Christophe Munyanderu, ambaye ni mshirikishi wa kundi la “Convention for the Respect of Human Rights” -(CRDH), anasema wapiganaji walioshukiwa kuwa wanachama wa kundi la “Allied Democratic Forces” -(ADF), waliwaua wakaazi na kuteketeza nyumba katika vijiji vya Kandoyi na Bandiboli, mkoani Ituri, Ijumaa jioni na pia mapema siku ya Jumamosi.

Also Read
Watu wawili wapatikana na aina mpya ya virusi vya Covid-19 Uingereza

Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya ki-demokrasia ya Congo huko Ituri, Jules Ngongo, alithibitisha kuuawa kwa takribani watu 20, na kusema majeshi ya serikali yamewaandama wavamizi hao. Kundi la “Allied Democratic Forces” -(ADF), ni la waasi wa Uganda waliohamia mashariki mwa Jamhuri ya ki-demokrasia ya Congo mapema miaka ya 1990.

Also Read
Jeshi la Uganda lashambulia waasi wa ADF nchini DRC

Usalama umezorota huko Ituri na pia katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini tangu serikali ilipotangaza utawala wa kijeshi katika mikoa hiyo miwili mwaka uliopita.

  

Latest posts

Janet Jackson Kuzindua Tena Albamu Yake ya Velvet Rope

Marion Bosire

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Marekani kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi