Watu 20 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kenya imenakili visa 20 zaidi vya Covid-19, baada ya kupimwa kwa sampuli 5,545 katika muda wa saa  24 zilizopita. Kiwango cha maambukizi ya Covid-19 hapa nchini sasa ni cha asilimia 0.4.

Idadi jumla ya visa vya maambukizi hapa nchini ni  322, 517 huku Idadi jumla ya sampuli zilizochunguzwa zikiwa 3, 304,677.

Also Read
Bunge la kaunti ya Nairobi latakiwa kurejelea vikao vya ana kwa ana

Kati ya visa hivyo vipya, watu 16 ni raia wa Kenya huku wanne wakiwa raia wa kigeni. Raia 15 ni wa kiume na watano ni wa kike.

Kulingana na Waziriwa afya Mutahi Kagwe, wagonjwa 37 wamepona virusi hivyo, ambapo 32 kati yao wametoka katika mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani na watano walitoka katika hospitali mbali mbali kote nchini. Idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni 302, 866.

Also Read
Uchaguzi Mkuu watajwa kuwa Chanzo cha ghasia katika sehemu kadhaa hapa nchini

Hakuna kifo ambacho kimeripotiwa katika muda wa saa 24 zilizopita, huku Idadi ya maafa ikisalia  5,632.

Also Read
Saitoti Torome: Athari za Covid-19 zilidumaza ukuaji wa uchumi wa Kenya

Hata hivyo wagonjwa 157 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini, wakati ambapo wagonjwa 647 wanatunziwa nyumbani.

Wagonjwa wanne wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, watatu kati yao wanatumia mitambo ya kuwasaidia kupumua na mmoja anapokea hewa ya ziada ya Oxygen.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi