Watu 22 watekwa nyara na majambazi nchini Nigeria

Takriban watu 22 wametekwa nyara katika kijiji cha Angwar Maji nchini Nigeria, siku moja baada ya mkuu wa polisi nchini humo kuzuru eneo hilo.

Wakazi wamesema majambazi waliovaa sare za jeshi na kujihami na silaha kali, walivamia eneo hilo siku ya Jumamosi usiku.

Also Read
Karim Khan achaguliwa kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya ICC

Yasemekana majambazi hao waliingia nyumba baada ya nyumba Jumapili usiku, wakiwachagua mateka, kabla ya kutoweka na wao.

Also Read
Davido Ampongeza Don Jazzy kwa Kusajili Msanii Aliyepata Umaarufu kwa Kuimba Wimbo wa Davido

Wanakijiji wengi walidhani huo ulikuwa msako wa kijeshi hadi pale walipofahamishwa na baadhi ya mateka waliofanikiwa kutoroka kwamba hao walikuwa majambazi.

Also Read
Wizara ya Elimu ya China yawapa nafuu wazazi wakati shule zinapofungwa kwenye likizo ndefu ya majira ya joto

Eneo hilo lililo karibu na barabara kuu ya Abuja –Kaduna linafahmika sana kwa visa vya utekaji nyara,vinavyotekelezwa na magenge ya majambazi yakitafuta pesa

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Marekani kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

Tom Mathinji

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Burkina Faso Paul-Henri Damiba ajiuzulu

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi