Watu 26 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Watu 26 zaidi wameambukizwa Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 2,621 katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufikisha idadi jumla ya visa vilivyothibitishwa hapa nchini kuwa 323,583.

Kulingana na taarifa kutoka wizara ya afya, kiwango cha maambukizi ya Covid-19 hapa nchini sasa ni cha asilimia 1.0, huku idadi jumla ya sampuli zilizochunguzwa ikiwa 3,554,588.

“Kati ya idadi hiyo watu 22 ni raia wa Kenya na wanne ni raia wa Kigeni. Waathiriwa 18 ni wa kiume na wanane ni wa kike. Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miaka mitanu na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 68,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Also Read
Uganda yakana madai kwamba viongozi wakuu serikalini wamechanjwa kisiri dhidi ya COVID-19

Kaunti ya Nairobi ilinakili visa 22, nazo Bungoma, Busia, Laikipia naUasin Gishu 1 zikiandikisha kisa kimoja kila kaunti.

Wagonjwa 19 zaidi wamepona virusi hivyo, 16 kati yao kutoka mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani na watatu waliruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini. Idadi jumla ya wagonjwa waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni 317,801.

Also Read
Watu 1,494 waambukizwa COVID-19 katika muda wa masaa 24 yaliyopita

Wakati huo huo mgonjwa mmoja zaidi amefariki kutokana na makali ya Covid-19 hapa nchini, hiki kikiwa kifo kilichoripotiwa kuchelewa baada ya ugaguzi wa rekodi za hospitali katika mwezi wa Aprili mwaka 2022. Idadi jumla ya maafa kutokana na Covid-19 hapa nchini sasa ni 5,649.

Jumla ya wagonjwa 11 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini, huku wengine 122 wakihudumiwa wakiwa nyumbani.

Also Read
Watu 1,183 zaidi wathibitishwa kuwa na Covid-19 hapa nchini

Hadi kufikia tarehe 11 mwezi Aprili mwaka 2022, jumla ya watu 17,766,932, walikuwa wamechanjwa dhidi ya Covid-19 kote nchini. Kati ya idadi hiyo, 16,251,169 wana umri wa miaka 18 na zaidi.

Vijana 1,227,855 walio na umri wa kati ya miaka 15 na 17, wamechanjwa dhidi ya virusi hivyo hapa nchini huku watu 287,908 wakipokea chanjo ya kuimarisha kinga dhidi ya Covid-19.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi