Watu 3 wafariki Mandera baada ya basi walilokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi

Watu watatu wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati basi walilokuwa wameabiri lilipokanyaga kilipuzi kwenye barabara ya Arabia, Kaunti ya Mandera.

Also Read
Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Basi hilo lilikuwa likielekea mjini Mandera kutoka Lafey wakati lilipokanyaga kilipuzi hicho, mapema leo.

Also Read
Walimu 330,000 wamerejea shuleni tayari kuwapokea wanafunzi Jumatatu

Gavana wa kaunti ya Mandera Ali Roba amethibitisha tukio hilo huku polisi wakisema wako katika hali ya tahadhari.

Also Read
Maafisa watatu wa polisi wajeruhiwa baada ya gari lao kushambuliwa Mandera

Waliojeruhiwa wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Mandera kwa matibabu.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi