Watu 30 watekwa nyara nchini Nigeria

Zaidi ya watu 30 wameripotiwa kutoweka katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria, baada ya kushambuliwa mwishoni wa wiki na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo.

Also Read
Boris Johnson awaandikia wabunge kuhusu kanuni mpya za COVID-19 Uingereza

Walioshuhudia wamesema wahasiriwa kutoka mji wa Rann, walifyatuliwa risasi na watu waliokuwa na bunduki wakiwa kwenye pikipiki walipokuwa wakienda msituni kutafuta kuni.

Hata hviyo baadhi ya watu walioshambuliwa walitoroka wakiwa na majeraha ya risasi. Inahofiwa kuwa watu wengine kadhaa wametekwa nyara au kuuawa.

Also Read
Waziri wa Afya wa Jordan afutwa kazi kufuatia vifo vya wagonjwa 7 waliokosa oksijeni

Haijabainika ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo, ingawa kundi la Boko Haram na kundi jingine la wanamgambo linaloaminika kuwa na uhusiano na lile Islamic State, yamekuwa yakiendesha shughuli zake katika eneo hilo.

  

Latest posts

Mataifa ya G7 kusitisha uagizaji dhahabu kutoka Urusi

Tom Mathinji

Mzozo wa Ukraine na Russia kujadiliwa katika mkutano wa G7

Tom Mathinji

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia augua Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi