Watu 3,000 ndio watahudhuria sherehe za Mashujaa uwanjani Gusii

Ni watu 3,000 pekee watakaoruhusiwa katika uwanja wa Gusii kuadhimisha siku kuu ya mashujaa ya mwaka huu itakayoandaliwa katika kaunti ya kisii, ili kudhibiti msambao wa virusi vya Covid-19

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa uwanja huo Jumatautu, katibu katika wizara ya usalama  Karanja kibicho, alisema hatua hiyo inakusudia kuhakikisha masharti ya kutotangamana yanatekelezwa pamoja na masharti mengine ya wizara ya afya ya  kudhibiti Covid-19.

Also Read
Prof. Magoha awaonya maafisa watundu katika baraza la KNEC

Kwa mujibu wa Kibicho runinga kubwa zitawekwa mjini kisii ambapo wananchi wataweza kufuatilia sherehe hiyo moja kwa moja itakayoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Kibicho alisema wanachama wa kamati hiyo waliozuru uwanja huo waliridhika na kiwango cha maandalizi ambacho kimetekelezwa.

Also Read
Marekani yaitaja China kuwa tishio kubwa kwa demokrasia duniani

Sherehe hiyo ndiyo ya kwanza kabisa kuandaliwa nchini tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha virusi vya Covid-19 humu nchini mwezi Machi ambapo serikali ilipiga marufuku hafla za umma kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae alisema ni heshima kubwa kwa kaunti hiyo kuandaa sherehe hiyo na kwamba kiwango cha matayarisho ni cha hali ya juu.

Also Read
Shule kadhaa Baringo huenda zisifunguliwe kesho kwa hofu ya mashambulizi

Siku kuu ya Mashujaa huadhimishwa kila tarehe 20 mwezi Octoba kuwaenzi waliochangia katika kupata uhuru wa nchi hii.

 

 

  

Latest posts

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Serikali yaongeza kafyu ya kuto-toka nje usiku katika kaunti tatu za Rift Valley

Tom Mathinji

Karua asema Muungano wa Azimio utahakikisha uongozi bora

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi