Watu 310 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Taifa hili limethibitisha visa 310 zaidi vya COVID-19  kutoka kwa  sampuli  3,961 zilizopimwa katika muda wa saa 24 zilizopita. Kiwango cha maambukizi cha sasa ni  asili-mia  7.8.

Miongoni mwa  walioambukizwa,  watu  256 ni raia wa kenya huku 54 wakiwa raia wa kigeni.

Mwathiriwa mdogo  zaidi ni mtoto wa umri wa  miezi minne huku wa umri  mkubwa zaidi akiwa na miaka 97.

Jumla ya visa  vilivyothibitishwa  kufikia sasa ni  317,634 navyo vipimo  viliovyofanya  kufikia  hadi  sasa vikifikia  3,147,823.

Also Read
Mwalimu mkuu achuguzwa kuhusiana na wizi wa Mtihani wa KCSE kaunti ya Narok

Hakuna  vifo vilivyoripotiwa katika kipindi hicho. Wagonjwa 3,384 wamepona ugonjwa huo, 3,329  kati yao kutoka Mpango wa  matibabu ya nyumbani  huku 55 wakiwa wa kutoka katika vituo mbalimbali vya afya kote  nchini.

Jumla ya watu waliopona  kufikia sasa ni 284,727, kati yao233,586wakiwa kutoka katika mpango wa matibabu  ya nyumbani, huku 51,141 wakitoka katika vituo mbalimbali vya afya nchini.

Kaunti ya Nairobi bado inaongoza kwa idadi ya maambukizi kwa visa 180, Siaya 16, Uasin Gishu 16, Kiambu 14, Migori 12, Nakuru nane Nandi saba, Nyamira na Kisii visa sita kila kaunti

Also Read
Serikali yajizatiti kuimarisha mifumo ya usafiri na uchukuzi kote nchini

Kaunti  tano zenye visa viwili vya  maambukizi ni pamoja na Garissa, Kajiado Nyeri na Laikipia, huku Machakos, Meru Mombasa, Murang’a na Taita Taveta zikiwa na  kisa  kimoja  kila moja.

Jumla ya wagonjwa  1,043 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini huku wengine  10,664 wakihudumiwa nyumbani.

Also Read
Afueni kwa wanaotafuta ajira baada ya kuondolewa hitaji la kuwa na stakabadhi za taasisi husika

Kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe, wagonjwa 53 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, 51 kati yao wanatumia mitambo ya kuwasaidia kupumua na wawili wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen.

Jumla ya watu  11,082,457  wamechanjwa dhidi ya Covid-19 hapa nchini, huku 6,198,816 wakichanjwa awamu ya kwanza na 4,763,682 wakichanjwa kikamilifu.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi