Watu 345 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kenya imenakili visa 345 vipya vya maambukizi ya Covid-19, kutoka kwa sampuli 6,686 zilizopimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hii inaashiria asilimia 5.2 ya maambukizi mapya. Watu 339 kati yao ni raia wa kenya na sita raia wa kigeni.

195 ni wanaume na 150 ni wanawake. Mwathiriwa wa umri mdogo zaidi ni mtoto wa umri wa miaka miwili ilhali wa umri wa juu zaidi ni mkongwe wa umri wa miaka 94.

Kwenye taarifa, waziri wa afya Mutahi Kagwe, alisema jumla ya idadi ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa kufikia sasa ni 160,904 na jumla ya visa vilivyothibitishwa tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huo humu nchini ni 1,688,106. 

Wagonjwa 140 wamepona ugonjwa huo 82 kutoka utunzi wa nyumbani na 58 kutoka hospitali mabali mbali.

Jumla ya wagonjwa waliopona ni 109,217 ambapo 79,525 ni kutoka utunzi wa nyumbani na 29,692 kutoka hospitali mbali mbali.

Jumla wa vifo 24 vimeripotiwa, 15 katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

Also Read
Monica Juma apigiwa debe kuwa katibu mkuu wa Jumuia ya Madola
Also Read
Wizara ya afya yaitisha shilingi bilioni 1.4 kuboresha uhifadhi wa chanjo ya covid-19

Jumla ya wagonjwa 2,805 wameaga dunia humu nchini kutokana na makali ya ugonjwa huo.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi