Watu 36 waorodheshwa kwa wadhifa wa makamishna wa IEBC

Jopo la uteuzi la tume huru ya uchaguzi na mipaka hapa nchini-IEBC limeorodhesha watu 36 kati ya 660 waliotuma maombi kujaza nafasi nne za makamishna wa IEBC zilizo wazi.

Mwenyekiti wa jopo hilo, Elizabeth Muli alisema kwenye taarifa kwamba mahojiano ya walioorodheshwa yatafanywa kuanzia tarehe 7 mwezi Julai hadi tarehe 22.

Also Read
Wanaounga mkono BBI wana muda hadi Jumatatu kudhibitisha maelezo yao

Majaribio ya kisaikolojia yatafanyiwa wawaniaji hao siku ya Jumatano Juni 30 kwa njia ya kuulizwa maswali, huku yale ya kujumuisha kielelezo cha kifani yakifanywa kati ya tarehe 7 hadi 22 mwezi Julai katika ukumbi wa KICC.

Jopo hilo limewaalika wananchi kuwasilisha taarifa zilizoandikwa au habari zozote muhimu kuhusiana na ustahiki wa wawaniaji hao kufikia Juni 25 mwaka huu.

Also Read
Wito watolewa wa hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wanasiasa wanaowatishia wanahabari

Miongoni mwa walioorodheshwa ni aliyekuwa mwanachama wa tume ya kitaifa ya huduma ya polisi Abdalla Mohamed, aliyekuwa naibu mwenyekiti wa bodi ya kusaili majaji na mahakimu Roseline Doreen Adhiambo Odhiambo Odede, aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya haki za binadamu Kagwigira Mbogori, Koki Muli na aliyekuwa kamishna wa tume ya maridhiano na mshikamano wa kitaifa-NCIC Joseph Gitile Naituli.

Also Read
Mahakama kutoa uamuzi leo kuhusu rufaa saba za kupinga BBI

Nyadhifa hizo ziliachwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa Roselyn Akombe, Paul Kurgat, Margaret Mwanchanya na Connie Maina baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi