Watu 388 waambukizwa COVID-19, wagonjwa sita waaga dunia

Idadi ya maambukizi ya COVID-19 humu nchini imefikia 41,546 baada ya watu wengine 388 kuthibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Hii inatokana na sampuli 4,287 zilizopimwa katika muda wa masaa 24 yaliyopita.

Kati ya visa hivyo vipya, 383 ni vya Wakenya ilhali vitano ni vya raia wa kigeni.

Also Read
Waititu afika Mahakamani kwa kesi ya ufujaji wa shilingi milioni 588

Wanaume walioambukizwa na 284 ikilinganishwa na 104 wanawake, wakiwa kati ya umri wa miaka mine hadi 85.

Kaunti ya Nakuru inaongoza kwa visa 86 ikifuatwa na Nairobi 84, Mombasa 51, Trans Nzoia 49, Kiambu 29, Kisumu 17, Kericho 11, Meru 10, Busia 10, Bungoma 8, Machakos 7, Garissa 5, Kajiado 3, Tharaka Nithi 3, Nyamira 3, Nyeri 2, Siaya 2, Makueni 2, Nandi 2, Kwale 2, na Nyandarua 2.

Also Read
Magoha afutilia mbali uwezekano wa shule kufungwa tena

Wagonjwa 63 wamethibitishwa kupona na kufikisha 31,000 idadi ya waliopona kutokana na ugonjwa huo.

Also Read
Mwenyekiti wa ODM kaunti ya Mombasa Mohammed Hatimy ameaga dunia

Kati ya hao 63, waliokuwa wakitibiwa nyumbani walikuwa 23 huku 40 wakiruhusiwa kuondoka kutoka vituo mbali mbali vya afya humu nchini.

Hata hivyo, wagonjwa sita wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi jumla ya waliofariki hadi 766.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi