Watu 57 wahukumiwa kuhudumia jamii kwa kukiuka masharti ya kudhibiti Covid-19

Watu 57 wamehukumiwa kuhudumia jamii kwa muda wa wiki moja na mahakama moja ya Kibra kwa kukiuka masharti ya wizara ya afya ya kudhibiti msambao wa Covid-19.

Watu hao walikamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Milimani Jijini Nairobi, kabla ya kuachiliwa chini ya uangalizi wa halmashauri ya Usimamizi wa jiji la Nairobi NMS, kwa kipindi hicho cha huduma kwa jamii.

Also Read
Jaji Marete Njagi asailiwa kwa wadhifa wa jaji Mkuu

Huku ikitoa hukumu hiyo, Mahakama hiyo ya Kibra ilisema halmashauri ya NMS,itasimamia shughuli hiyo katika taasisi mbali mbali na mitaa ya Jiji la Nairobi.

Also Read
KCAA yasimamisha safari za ndege kati ya Kenya na Somalia

Watu hao 57 wanatarajiwa kuripoti kutoa huduma hiyo kwa jamii saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni kila siku.

Majukumu yao yanajumuisha kusafisha soko la Marikiti na lile la Muthurwa, mzunguko wa Globe,mto Nairobi pamoja na majukumu mengine jinsi watakavyoelekezwa.

Also Read
Taifa hili lashuhudia ongezeko la idadi ya wanaopona Covid-19

Aidha wale watakaokiuka watakamatwa upya na kushtakiwa kisha wataadhibiwa vikali Kulingana na taarifa ya halmashauri ya NMS.

  

Latest posts

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi