Watu 945 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Taifa hili linazidi kunakili Idadi ya juu ya visa vya Covid-19 huku watu 945 zaidi wakithibitishwa kuwa na virusi hivyo baada ya kupimwa kwa sampuli 7,295 katika muda wa saa 24 zilizopita. Kiwango cha maambukizi ya Covid-19 hapa nchini sasa ni cha asilimia 13.

Kati ya visa hivyo vipya watu 910 ni raia wa Kenya ilhali  35 ni raia wa kigeni huku 481 wakiwa wanaume na 464 wakiwa wanawake. Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miezi 11 huku mkongwe zaidi ana umri wa miaka 100.

Idadi jumla ya visa vya Covid-19 vilivyothibitishwa hapa nchini sasa ni 201,954 na Idadi jumla ya sampuli zilizochunguzwa ni  2,124,274.

Also Read
Kenya yaripoti visa 431 vipya vya maambukizi ya COVID-19

Taarifa kutoka kwa wizara ya afya, inaashiria kuwa kaunti ya Nairobi ilinakili visa 416, Mombasa 73, Kiambu 72, Kilifi 52, Nakuru 43, Kajiado 33, Uasin Gishu 29, Makueni 28, Machakos 26, Murang’a 25, Kitui 13 nazo Busia, Baringo na  Kericho zikiandikisha visa 12 kila kaunti.

Kirinyaga na Migori zilinakili visa 11 kila moja , Lamu 9, Siaya 8, Garissa 8, Homa Bay 7 huku Kisumu, Nyandarua na Trans Nzoia zikiwa na visa 5 kila moja.

Narok iliandikisha visa 4, Nyeri 3, Kisii 3, Kakamega 3, West Pokot 3, Marsabit 2, Bungoma 2, Taita Taveta 2, nazo Elgeyo Marakwet, Kwale, Laikipia, Mandera, Meru, Vihiga, Bomet na Isiolo zikiandikisha kisa kimoja kila kaunti.

Also Read
Tume ya EACC na shirika la KBC zashirikiana katika vita dhidi ya ufisadi

Taarifa hiyo pia ilidokeza kuwa watu 216 zaidi wamepona ugonjwa huo, 152 kati yao kutoka mpango wa utunzi wa nyumbani na 64 kutoka hospitali mbali mbali kote nchini.

Idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni 188,438 huku 150,195 wakitoka mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani na 38,243 walitoka katika hospitali mbali mbali kote nchini.

Lakuhuzunisha ni kwamba watu 16 zaidi wamefariki kutokana na makali ya Covid-19 hapa nchini,vyote vikiwa vifo vilivyoripotiwa kuchelewa baada ya ukaguzi wa takwimu za hospitali katika tarehe tofauti katika miezi ya Machi, Aprili, Juni na Julai mwaka 2021.

Also Read
Idadi ya wanaojitokeza kutoa damu humu nchini yadidimia

Jumla ya wagonjwa 1,432 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini ilhali wengine 3,975 wanahudumiwa nyumbani. Wagonjwa 175  wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, 41 kati yao wakitumia mitambo ya kuwasaidia kupumua na 82 wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen. Wagonjwa 52 wangali wanachunguzwa.

Hadi kufikia tarehe 29 mwezi Julai mwaka 2020, watu 1,712,550 wamechanjwa dhidi ya Covid-19 kote nchini. Watu  1,058,280 walichanjwa katika awamu ya kwanza 654,270 walichanjwa katika awamu ya pili.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi