Watu wanne wafariki katika ajali ya barabarani Bungoma

Watu wanne walifariki Alhamisi usiku baada ya matatu waliokuwa wakisafiria kugongana na lori aina ya trela katika eneo la Mayanja kwenye barabara kuu ya kutoka Bungoma hadi  Malaba.

Kulingana na walioshuhudia, watu wawili walifariki papo hapo ilhali wengine wawili walifariki walipowasili katika hospitali ya kutoa huduma maalum za matibabu ya kaunti ya Bungoma.

Also Read
Bunge lapendekeza kuanzisha kituo chake cha habari

Waliofariki walijumuisha dereva wa matatu hiyo.  Watu wengine watano wamelazwa hospitalini.

Aliyeshuhudia ajali hiyo ambaye alikuwa akiendesha gari lake nyuma ya matatu aliliambia shirika la utangazaji nchini-KBC kwamba ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa mbili usiku wakati lori lililokuwa likitoka upande ule mwingine lilipojaribu kupita gari lingine na kugonga matatu hiyo.

Also Read
Kiwanda cha kusafisha mafuta cha kipevu chakaribia kukamilika

Akithibitisha ajali hiyo, kamanda wa trafiki katika kaunti ya Bungoma, Inspekta Simon Irungu, alisema mabaki ya matatu hiyo yamekokotwa hadi kituo cha polisi cha Bungoma huku mipango ikifanywa ya kukokota trela hiyo hadi kituo hicho cha polisi.

Also Read
KBC yakashifu kuondolewa kwa mwanahabari wake katika mdahalo wa wagombea wenza wa Urais

Dereva wa lori hilo amekamatwa huku polisi wakianzisha uchunguzi kuhuu ajali hiyo.

  

Latest posts

Japhet Koome ateuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi

Tom Mathinji

Majukumu ya Naibu Rais Rigathi Gachagua yabainishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi ateuliwa waziri mwenye Mamlaka zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi