Watu watano wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wakili Willie Kimani

Maafisa wanne wa Polisi na raia mmoja wana kesi ya kujibu kuhusiana na mauaji ya wakili Willie Kimani, Josephat Mwenda na dereva  Joseph Muiruri tarehe 23 mwezi Juni mwaka 2016.

Lady Justice Jessie Lessit katika uamuzi wake alisema ameshawishiwa na upande wa mashtaka kwamba maafisa wa polisi Fredrick Leliman, Stephen Cheburet, Sylvia Wanjiku, Leonard Mwangi na raia Peter Ngugi Wana kesi ya kujibu dhidi ya watatu hao.

Also Read
IEBC yawaidhinisha wagombeaji 9 katika uchaguzi mdogo wa Msambweni

“Baada ya kutathmini ushahidi uliotolewa, nimeafikia uamuzi kwamba upande wa mashtaka umedhihirisha washtakiwa Wana kesi ya kujibu,” alisema Justice Jessie Lessis.

Upande wa mashtaka ulitoa ushahidi dhabiti jinsi watano hao walivyowateka nyara Willie, Josephat, na Joseph tarehe June 23, 2016, baada yao kuondoka katika Mahakama ya Maviko walikohudhuria kesi moja iliyohusisha mmoja wa washtakiwa Jao.

Baada ya msako uliodumu wiki moja, miili ya watatu hao ilipatikana katika mto Athi eneo la  Ol Donyo Sabuk kaunti ya Machakos.

Also Read
Jaji Mkuu Martha Koome awahimiza majaji kutekeleza majukumu bila hofu

Kesi hiyo ilianza kusikizwa mwaka 2016 huku upande wa mashtaka ukikamisha kuskizwa kwake baada ya kuwahoji mashahidi 46.

Miongoni mwa waliotoa ushahidi ni pamoja na maafisa wa polisi, wafanyikazi wenza wa Willie, mashahidi waliopata miili hiyo mtoni mwendeshaji mmoja wa Boda Boda ambaye upande wa mashtaka ulimtaja alizungumza mara ya mwisho na Willie Kimani na ambaye pia alichukua kijikaratasi kilichokuwa na ujumbe kutoka kwa wakili huyo.

Also Read
Oparanya aibuka Gavana mchapa kazi bora zaidi

Vile vile upande wa mashtaka ulipokea ushahidi kupitia kwa maandishi kutoka kwa shahidi wa tano Peter Ngugi, ulioelezea jinsi mauaji hayo yalivyopangwa na kutekelezwa.

Upande wa mashtaka pia ulitumia teknolojia zilizohusisha sampuli za DNA na data za simu ili kudhibitisha kesi dhidi ya watano hao.

Upande wa utetezi utaanza kujitetea kuanzia tarehe 27 mwezi Septemba mwaka 2021.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi