Watu watatu wafariki baada ya kanisa kuporomoka Nigeria

Yamkini watu watatu wakiwemo watoto wawili wamefariki baada ya jengo la kanisa moja kuporomoka kusini mwa Nigeria.

Kanisa hilo liliporomoka Jumanne Usiku, wakati wa ibada ya jioni katika mtaa duni wa Ok-panam eneo la Asaba, katika makao makuu ya jimbo la Delta.

Also Read
Chanjo dhidi ya Ebola yawasili nchini Guinea

Hayo ni kulingana na msemaji wa polisi Bright Edafe. Watu 11 ,kati ya 18 waliookolewa wanaendelea kupokea matibabu.

Kulingana na vyombo vya habari, kanisa hilo liliporomoka wakati maombi ya jioni yakiendelea.

Also Read
Visa 550 zaidi vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Kuporomoka kwa majengo ni tukio la kawaida nchini Nigeria ambako mamilioni ya watu wanaishi kwenye mitaa duni, huku kanuni za ujenzi, zikikiukwa maksudi.

Also Read
Uhispania yatangaza hali ya hatari kutokana na awamu ya pili ya maambukizi ya Corona

Taasisi ya kudhibiti ujenzi nchini humo imekuwa ikiangaziwa pakubwa baada ya jengo moja refu lililokuwa likijengwa  kuporomoka jijini Lagos mwezi novemba mwaka jana, na kuua watu 45.

  

Latest posts

Washukiwa wawili wakamatwa na pembe za ndovu kaunti ya Busia

Tom Mathinji

Shujaa yaipakata Canada alama 24-5 katika msururu wa Seville Uhispania na kufufua matumini ya kutinga robo fainali

Dismas Otuke

Serikali ya Mombasa yalaumiwa kwa kushindwa kufunga jaa la taka la VOK

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi