Watu wawili wauawa kwa kupigwa risasi Baragoi

Taharuki imetanda eneo la Baragoi katika kaunti ndogo ya Samburu kaskazini baada ya watu wawili kuuawa Jumatatu kwenye mashambulizi mawili tofauti.

Mwathiriwa wa kwanza ambaye ni mvulana wa miaka tisa aliaga dunia papo hapo baada ya kugongwa na risasi kifuani alipokuwa akichunga mifugo katika eneo la Natiti mwendo wa saa tano asubuhi.

Also Read
Serikali kusuluhisha tatizo la jadi kuhusu ardhi kupitia utoaji hatimiliki

Na wakati wa jioni, mhudumu mmoja wa boda boda na abiria wake walijeruhiwa vibaya katika kile kinachoaminika kuwa shambulizi la kulipiza kisasi mjini Baragoi.

Also Read
Mwanaume amuua mamake kabla ya kujitoa uhai katika kaunti ya Samburu

Afisa mmoja wa afya katika hospitali ya kaunti ndogo ya Baragoi, Simon Kanguro amesema kuwa mhudumu huyo wa bodaboda aliaga dunia baadaye kutokana na majeraha aliyoyapata.

Also Read
Kenya yajiandaa kukabiliana na wimbi la pili la uvamizi wa nzige

Kanguro alisema kuwa abiria naye bado amelazwa kwenye hospitali hiyo ingawa yu thabiti.

Wakazi wa eneo hilo sasa wanatoa wito kwa mashirika ya usalama kuchukua hatua za dharura zitakazowezesha kukamatwa kwa washukiwa waliotekeleza mashambulizi hayo mawili.

 

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi