Watu wawili zaidi wafariki hapa nchini kutokana na Covid-19

Watu wawili zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa COVID 19 katika kipindi cha saa 24 zilizopita, na kufikisha 5,651 idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo hapa nchini.

Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo hapa  nchini sasa ni cha asilimia 0.9, baada ya kuthibitishwa kwa visa vipya 20 kutoka sambuli 2,219 zilizofanyiwa uchunguzi katika kipindi cha 24, zilizopita

Idadi ya jumla ya wale walioambukizwa ugonjwa huo kufikia sasa ni 324,242 kutoka sambuli 3,649,319.

Wagonjwa 13 zaidi wamepona ugonjwa huo, wote hao kutoka mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani.

Also Read
Kenya yanakili visa 29 vipya vya Covid-19
Also Read
Monica Juma apigiwa debe kuwa katibu mkuu wa Jumuia ya Madola

Wagonjwa watatu wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya, huku wengine 312 wakihudumiwa wakiwa nyumbani.

Kulingana na taarifa ya Waziri wa afya Mutahi Kagwe,kufikia tarehe 20 mwezi huu wa Mei, jumla ya watu18,081,205 walikuwa wamepokea chanjo ya covid-19.

Kati ya Idadi hiyo, watu 13,994 walichanjwa dhidi ya Covid-19, katika muda wa saa 24 zilizopita.  Kulingana na wizara ya afya, Asilimia 30.8 ya wakenya wamepokea chanjo kikamilifu dhidi ya Covid-19.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi