Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Kamishna wa kaunti ya Kitui, Thomas Sankei, amehimiza watumishi wa umma kuzingatia mfumo wa ushirikiano baina ya taasisi mbali mbali badala ya kutengana ili kufanikisha majukumu yao.

Akiongea huko Kitui baada ya kuongoza mkutano kuhusu utoaji huduma katika kaunti hiyo, Sankei alisema ushirikiano baina ya taasisi mbali mbali umedhihirisha manufaa yake wakati wa kampeini za nyumba hadi nyumba, hata kusababisha asilimia 98 ya wanafunzi waliokamilisha elimu ya msingi kujiunga na sekondari.

Also Read
Wakazi wa Rapso kaunti ya Isiolo wailaumu serikali kwa utovu wa Usalama
Also Read
Zoezi la utoaji chanjo dhidi ya Poli katika kaunti 13 kuanza mwishoni mwa wiki

Alitaka kuwe na ushirikiano kamili kuhusu shida zinazokabili wananachi kama vile utoaji hati za kuzaliwa, akiongeza kwamba kucheleweshwa kwa huduma hizo kunachangia ufisadi mkubwa miongoni mwa watumishi wa umma.

Also Read
Polisi wakomesha mkutano wa kisiasa Kitui

Alihimiza watumishi wa umma wawe wakijikadria wao wenyewe na kufikiria jinsi wanavyochukuliwa na wakenya wanaowahudumia.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi