Wauguzi watishia kuandaa maandamano ya kitaifa Jumatatu ijayo

Wauguzi wametishia kuandaa maandamano katika matawi yote kote nchini kuanzia Jumatatu ili kushinikiza baraza la magavana kusikiliza malalamishi yao.

Wauguzi hao wamesema maandamano hayo yataendelea hadi serikali za kaunti zote zitie saini masharti ya kurejea kazini ambayo yameafikiwa tayari kabla ya wao kurejea kazini.

Akihutubia wanahabari katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha wauguzi hapa nchini Seth Panyako alisema kigezo cha magavana kuwa matakwa yao hayawezekani kutekelezwa hakina msingi na kusema wauguzi watasalia mgomoni  hadi matakwa yao yashughulikiwe.

Also Read
Madaktari kuanza mgomo wao Jumatatu huku wauguzi nao wakidinda kurejea kazini

Wakati huo huo, wahudumu wa matibabu wanaogoma katika kaunti ya Mombasa wamedumisha msimamo wao wa kutorejea kazini hadi serikali ya kaunti hiyo na tume ya utumishi wa umma ya kaunti hiyo zishughulikie kikamilifu malalamishi yao.

Also Read
Wizara ya Afya yathibitisha maambukizi mapya 153 ya korona

Wakihutubia wanahabari mjini n Mombasa, katibu wa tawi la Mombasa la chama cha kitaifa cha wauguzi hapa nchini-KNUN Peter Maroko na mwenzake wa chama cha maafisa wa kliniki hapa nchini Franklin Makanga, walisema makubaliano hayo ya tarehe 19 mwezi huu na mwajiri wao hayajatekelezwa na hakuna maelezo  bayana kuhusu ni lini yatatekelezwa.

Also Read
Chebukati atetea gharama ya kuandaa kura ya maamuzi ya shilingi bilioni 14

Wahudumu hao wa matibabu wanataka kupatiwa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona, kupewa marupurupu ya kuhatarisha maisha yao, bima ya matibabu kwa wanachama wote na kupandishwa vyeo miongoni mwa matakwa mengine.

Haya yanajiri huku mgomo wa kitaifa wa wahudumu wa matibabu ukiingia siku ya 46.

  

Latest posts

Uhaba wa maji wakumba kaunti ndogo ya Lagdera baada ya kukauka kwa vidimbwi

Tom Mathinji

Magoha: Serikali haitabatilisha agizo lake kuhusu utumiaji wa mabasi ya shule.

Tom Mathinji

Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi