Waumini wa Kanisa la Shianda wahakikishiwa kufanyika kwa mchango wa Ruto

Mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali leo amewashakikishia waumini wa Kanisa Katoliki la Shianda kuwa hafla ya kuchangisha pesa itafanyika katika muda usiozidi miezi miwili.

Hii ni baada ya hafla hiyo iliyokuwa iongozwe na Naibu Rais William Ruto kutibuka kwa sababu ya kutotimiza kanuni mpya za kudhibiti mikutano ya hadhara zilizotangazwa na baraza la ushauri kuhusu usalama wa kitaifa.

Also Read
Kanisa Katoliki lashtumu hatua ya sekta ya Uchukuzi kubeba Idadi kamili ya abiria

Washiali aliyeandamana na aliyekuwa Seneta wa Kakamega Boni Khalwale amesema wanasiasa kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya wanaomuunga mkono Naibu Rais wamejitolea kuziba pengo kubwa lililopo kati ya maskini na matajiri.

Also Read
Waalikwa 4,000 tu kuruhusiwa Uwanjani Gusii kwa sherehe za Mashujaa

Ruto alitarajiwa kuongoza mkutano wa kuchangisha pesa katika sehemu hiyo lakini ukafutiliwa mbali na afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Shiada kutokana na kile alichosema ni kutotimiza masharti yaliyowekwa kuhusu maandalizi ya mikutano ya kisiasa ambayo ni pamoja na kupata kibali cha polisi siku tatu kabla ya mkutano kuandaliwa.

Also Read
Ruto akutana na mgombea huru wa uchaguzi mdogo wa Msambweni, Feisal Bader

 

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi