Wazazi wa watoto wenye ulemavu wahimizwa kutowabagua

Wazazi wenye watoto walemavu katika Kaunti ya Wajir na maeneo ya karibu wamehimizwa kuwapa watoto wote fursa sawa licha ya hali zao.

Haya yanajiri wakati baadhi ya wazazi wa watoto walio na ugonjwa wa kupooza kwa ubongo kuwaficha wakisema hali hiyo ni laana, hali ambayo inaweza kusababisha vifo vya watoto kama hao.

Also Read
Mawaziri wa kaunti nao wanadai kuongezwa mishahara na marupurupu

Kituo cha kuwatunza watoto hao cha Misheni ya Kanisa Katoliki ya Wajir ambacho hupokea na kushughulikia matibabu ya watoto hao kimesifiwa kwa juhudi zake za kushughulikia watoto wenye tatizo hilo ambalo husababishwa na jeraha kwa ubongo au matatizo ya ujauzito.

Also Read
DCI yawakamata washukiwa wanaolaghai watu kwa kigezo cha kuwatafutia wapenzi

Akiongea na wanahabari wa kituo cha Televisheni Cha KBC Channel 1, Mtawa Jenipher Mosima ambaye anasimamia kituo hicho alisema watoto wenye ulemavu sio laana na wana haki ya kupata mahitaji yote ya kimsingi kama watoto wengine.

Also Read
Wandani wa Ruto wamtaka Jaji Mkuu Martha Koome kujiondoa katika kamati ya maandalizi ya uchaguzi

Mosima alisema kutokana  na janga la COVID-19, watoto hao wamo kwenye hatari ya kuambukizwa ikiwa wazazi wao hawazingatii kanuni za kiafya.

Aliwahimiza wazazi kutunza watoto wa aina hiyo vizuri na kutokata tamaa kuwatunza.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi