Waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed amepokea ripoti kuhusu dhuluma za kijinsia na unyanyasaji wa wanamichezo kutoka kwa kamati iliyokuwa ikitiyarisha ripoti hiyo ikiongozwa na mwanariadha mstaafu Catherine Ndereba.
Ndereba ameelezea matumaini yake kuwa ripoti hiyo itachangia kupunguza dhuluma za kijinsia na unyanyasi michezoni.
Waziri Amina amesema kuwa kamati hiyo imetoa hoja na mapendekezo mengi kulingana na uchunguzi uliofanywa huku ripoti hiyo ikitarajiwa kuongoza warsha ya siku tatu itakayoandaliwa katika mkahwa wa Diani kuanzia tarehe 17 mwezi huu .

“Nimefurahishwa na uchunguzi na utathmini pamoja na mapendekezo yaliyotolewa na kamati hii huku baadhi ya ufichuzi uliotolewa ukitisha sana,na natumai ripoti hii itasaidi pakubwa kwenye warsha ya siku tatu itakayoandaliwa kuanzia tarehe 17 mwezi huu katika mkahawa wa Diani”akasema Amina
Kulingana na waziri Amina ripoti hiyo imeelezea baadhi ya changamoto zilizo michezoni kama vile wanawake kupokea malipo dunia ikilinganishwa na wanaume,upungufu wa makocha wa kike,kudhulumiwa kwa wanawake,ubaguzi wa kuangaziwa kwa wanamichezo wa kike kwenye vyombo vya habari miongoni mwa maswala mengine.

Waziri amesema kuwa wanamichezo 100,50 wa kike na 50 kiume sawia na maafisa wawili kutoka kila shirikisho wakiwa mwanaume mmoja na mwanamke mmoja watahudhuria warsha hiyo.
Kauli mbiu ya warsha hiyo itakuwa leveling the playing field:gender inclusivity in sports.