Waziri Amina ateuwa kamati ya mpito ya FKF ya watu 12 kuongoza soka kwa majuma matano

Waziri wa Michezo Dkt. Amina Mohammed ameteua kamati ya mpito ya watu 12 kuendesha soka nchini kwa kipindi cha majuma matano .

Kwenye gazeti rasmi la serikali   nambari 5518 ,waziri Amina amesema kuwa kamati hiyo ya muda itatekeleza majukumu yake kwa kipindi cha majuma matano  kuanzia Mei 11  .

Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya muda iliyokalisha muda wake mapema wiki hii  jaji mstaafu Aaron Ringerera  ndiye mwenyekiti wa tume hiyo ya mpito akisaidiwa na  Maurice Oyugi  atakayekuwa naibu mwenyekiti.

Also Read
Mwanafunzi wa zamani wa Moi Girls ahukumiwa miaka mitano gerezani

Wanachama wengine kwenye kamati hi ni Ali Amour, Bobby Ogolla, Neddy Atieno, Ceasar Handa
Hassan Haji, mchezaji mstaafu Dkt J. J. Masiga, Michael Muchemi, Rachael Kamweru, Mwangi Muthee na Anthony Isayi.

Afis ya kamati hiyo itaongozwa na Lindah Oguttu  huku Lorine Nerea  akiwa katibu.

Wanachama wengine wa afisi hiyo ni mwanahabari wa  michezo wa KBC Maxwell Wasike, Edward Rombo, Robin Toskin na Rashid Shedu.

Also Read
Rais Kenyatta awasili nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika

Kamati hiyo imejukumiwa  kutekeleza:-

(1) Kuendesha shughuli za shirikisho la  kandanda nchini kwa mjibu wa katiba ya FKF .

(2) Kuhakikisha shirikisho la soka nchini  lisamimia soka kwa mjibu wa sheria za michezo za mwaka 2013 .

(3) Kuongoza na kuhakikisha  soka ya Kenya inaendeshwa  bila tashwishwi ikiwemo kuandaa timu za taifa kwa mashindano ya humu nchini na yale ya kimataifa .

Also Read
Ligi kuu nchini Rwanda yasimamishwa na serikali

(4)Kusimamia na kuwezesha uidhinishaji wa katiba rasimu ya FKF.

Kulikuwa  na hofu kuhusu kukwama kwa soka ya humu nchini kufuatia kukamilika kwa makataa ya miezi sita ya kamati ya muda ya FKF iliyowasilisha ripoti kwa Waziri wa Michezo Dkt. Amina Mohammed mapema wiki hii.

 

  

Latest posts

Wahasibu watakiwa kufichua ufisadi bila uwoga

Tom Mathinji

Waakilishi wa Kenya ,Prisons na KCB wasajili ushindi wa pili mashindano Afrika kwa Voliboli ya vidosho

Dismas Otuke

Kenya na Zimbabwe zafungiwa nje ya mechi za kufuzu kombe la AFCON mwaka ujao nchini Ivory Coast

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi