Waziri Amina avunja FKF na kubuni kamati

Waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed amevuynjilia mbali shirikisho la soka nchini FKF na kuunda kamati ya muda itakayoongozwa na jaji mstaafu Aaron Ringera.

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari ameunda kamati ya watu 15 itakayosimamia soka kwa miezi 6 ijayo kabla ya kupisha uchaguzi mpya.

Also Read
Safari ya Gor kwenda Algeria yakumbwa na misukosuko

Amina ametaja sababu za kuunda kamati ya muda ya kuendesha soka kuwa matumizi mabaya ya pesa na Nick Mwendwa kufuatia uchunguzi wa mahesabu uliofanywa na msajili wa michezo Rose Wasike.

Also Read
Bondia Usyk ambwaga Anthony Joshua na kuhifadhi taji ya uzani wa Heavy

Kamati hiyo iliyoundwa inawajumuisha watu 15 wenye uzoevu wakiongozwa na jaji mstaafu Aaron Ringera huku wanachama wengine wakiwa Jenerali mstaafu Moses Oyugi,Fatma Adan,Philip Musyimi,Athony Isayi,Elisha Kiplagat,Hassan Haji,Fredrick Lekesike,waliokuwa wenyeviti wa chama cha raga nchini Mwangi Muthee ,na Richard Omwela,Neddy Okoth,,Ali Amour,Titus Kasuve,Bobby Ogola na J j Masiga.

Also Read
Gor Mahia walikuwa 'Bize' Sokoni huku dirisha la uhamisho wachezaji likifungwa

Waziri pia ameweka bayana kuwa wviongozi wa FKF wanapaswa kung’atuka afisini ili kuruhusu uchunguzi ufanyike na tayari ameifahamisha FIFA kuhusu mwelekeo huo.

  

Latest posts

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Wabunge wa kaunti ya Kitui wataka baa la njaa kutangazwa janga la kitaifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi