Waziri Amina kufika mbele ya kamati ya Senate Alhamisi

Waziri wa michezo Dkt Amina, atafika mbele ya kamati ya bunge la senate  inayosimamia wafanyikazi na hudumaa za kijamii Alhamisi,  asubuhi kuelezea songombwingo kati yake na shirikisho la soka nchini FKF.

Waziri ambaye atahudhuria kikao hicho kupitia mtandaoni anatarajiwa kutoa mwanga kuhusu ukaguzi wa akaunti za FKF uliofanywa maajuzi .

Also Read
Rais wa Zambia anatarajiwa hapa nchini Jumatano kwa ziara ya kiserikali

Amina pia atafafanua kuhusu ufadhili  kwa Harambre Stars kutoka kwa afisi yake,  na kueleza kuhusu matokeo ya uchunguzi wa matumizi ya fedha, zilizotolewa kwa FKF ndani ya miaka miwili iliyopita.

Afisi ya msajili mkuu wa michezo Rose  Wasike, iliwasilisha matokeo ya ripoti ya uchunguzi wa matumizi ya pesa mapema wiki hii kwa waziri Amina.

Also Read
Uchukuzi wa umma watakiwa kuzingatia masharti ya kudhibiti Covid-19

Kamati hiyo inaongozwa na seneta wa Nairobi Jonhstone Sakaja.

Kinara wa FKF  Nick Mwendwa amekuwa kwenye vita vikali vya maneno dhidi ya waziri , hivi punde ikiwa Jumanne usiku aliporopokwa kuwa waziri Amina  amekuwa akimhujumu.

Also Read
Gor yalala chali nyumbani mbele ya Mwarabu CR Belouizdad Nyayo

Endapo patatokea dosari zitajazoashiria ubadhirifu wa pesa , utakuwa ushindi kwa Waziri Amina, na mwanzo wa safari ya kumng’atua afisini ‘bosi’ wa soka Kenya Nicholas Kithuku Mwendwa.

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Tume ya EACC yachunguza wizi wa shilingi milioni 72 za kaunti ya Siaya

Dismas Otuke

Watu 171 wafariki kwenye mkanyagano wakati wa mechi ya soka nchini Indonesia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi