Waziri Amina kukagua matayarisho ya Chuo kikuu cha Kenyatta kwa mashindano ya riadha ya dunia ya U20

Waziri wa Michezo Dkt Amina Mohammed siku ya Alhamisi atazuru chuo kikuu cha Kenyatta ,kufanya ukaguzi wa maandilizi kwa mashindano ya dunia ya riadha kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20.

ukarabati wa uwanja wa Kasarani

Amina atazuru chuo hicho mida ya saa sita adhuhuri ambapo atakagua ukarabati wa mabweni ya chuo hicho yatakotumiwa na wanariadha na maafisa wao watakapokuwa wakilala wakati wa mashindano hayo ya siku tano.

Also Read
Kenya yaipiga kumbo Sudan na kutinga nusu fainali Cecafa

 

Pia uwanja wa mazoezi umekuwa ukikarabatiwa chuoni humo .

Wanariadha kutoka mataifa 128 watapiga makazi yao chuoni humo wakati wakati wa mashindano ya dunia yatayoandaliwa kati ya Agosti 17 na 22 .

 

Ziara hiyo inafuatia nyingine sawa na hiyo aliyoifanya waziri Amina siku ya Jumatano katika uga wa Kasarani alipokagua ukarabati na ujenzi unaoendelea .

Also Read
Mancity yatinga fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza
Waziri Amina akiwa na Ceo wa mashindano ya dunia ya U 20 Mike Rabar(katikati) na katibu katika wizara ya michezo Joe Okudo

Zikisalia siku 31 kabla ya kuanza kwa mashindano , matayarisho mengi yamo katika haua za lala salama.

Kenya ilitwikwa maandalizi ya mashindano hayo ya dunia baada ya kuandaa kwa njia ya kufana yale ya mwaka 2017 kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 18.

Also Read
Madereva 30 kushiriki mashindano ya WRC Safari Rally kati ya Juni 24-27

Kenya itakuwa ikiwania kuhifadhi taji ya jumla iliyotwaa katika makala ya mwaka 2018 mjini Tampere Finland ,kwa medali 11,dhahabu 6 fedha 4 na shaba 1.

Jamaica na Ethiopia ziliambatana katika nafasi za pili na tatu mtawalia kwa dhahabu 4 na 3 katika usanjari huo, wakati Afrika Kusini ikizoa pua dhahabu 3.

  

Latest posts

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Gatlin na Omanyala tayari kuonyesha ubora wao Kip Keino Classic Jumamosi

Dismas Otuke

FKF yakosolewa kwa kumtimua kocha Jacob Mulee wakati usiofaa

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi