Waziri Kagwe alaumu wanasiasa kwa kupotosha Wakenya kuhusu kanuni za COVID-19

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amewakashifu viongozi wa kisiasa kwa kuwa mfano mbaya kwa Wakenya katika uzingatiaji wa kanuni za kuzuia msambao wa COVID-19.

Kagwe amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kuwa kielelezo chema lakini tabia ya baadhi yao ya kuitisha mikusanyiko ya watu kwenye mikutano ya kisiasa bila kuzingatia kanuni za Wizara ya Afya inayolemaza vita dhidi ya COVID-19.

Akizungumza kutoka Makao Makuu ya Wizara ya Afya jijini Nairobi wakati wa kutoa taarifa ya siku kuhusu hali ya COVID-19 humu nchini baada ya kikao na Kamati ya Kitaifa ya kukabiliana na janga la korona, Waziri Kagwe amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la visa tangu kulegezwa kwa baadhi ya kanuni za COVID-19.

Also Read
Wakenya waonywa dhidi ya vyeti bandia vya COVID-19 huku visa vipya 1,554 vikiripotiwa

Kagwe amesema kiwango cha maambukizi sasa kimefikia asilimia 13, kikiwa ni cha juu zaidi kikilinganishwa na asilimia nne mwanzoni mwa mwezi huu.

Waziri huyo ameonya kuwa hali ya maambukizi sasa ni ya kutisha na kwamba nchi hii inashuhudia wimbi jipya la maambukizi.

Kuhusu takwimu za COVID-19 za masaa 24 yaliyopita, watu 685 zaidi wameambukizwa virusi hivyo na kufikisha 44,881, idadi ya jumla ya maambukizi humu nchini.

Also Read
Watu 1,166 zaidi wathibitishwa kuwa na Covid-19 hapa nchini

Visa hivi vimetokana na upimaji wa sampuli 4,912 na kufikisha jumla ya sampuli zilizopimwa kufikia sasa kuwa 621,976.

Kati ya visa hivyo vipya, 635 ni vya Wakenya na 50 ni vya raia wa kigeni; wanaume 456 na wanawake 229. Mwenye umri wa chini zaidi ni mtoto wa mwaka mmoja huku mkongwe zaidi akiwa na miaka 99.

Wagonjwa 105 pia wamethibitishwa kupona ambao 73 kati yao walikuwa kwenye mpango wa kuhudumiwa nyumbani huku 32 wakiruhusiwa kuondoka kutoka vituo vya afya.

Also Read
Mshukiwa wa kupeperusha droni nyumbani kwa Ruto aachiliwa kwa dhamana

Jumla ya waliopona kufikia sasa imefika 31,857.

Hata hivyo, wagonjwa saba wameaga dunia kutokana na makali ya ugonjwa huo na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kuwa 832.

Waziri Kagwe ametaja Kaunti za Nakuru, Kilifi, Turkana, Trans Nzoia, Kisii, Kisumu na Bungoma kuwa zinashuhudia ongezeko kubwa la maambukizi.

Ametoa wito kwa Wakenya kuwa makini zaidi katika kuzingatia kanuni hasa wakati huu ambapo shule zimefunguliwa.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi