Waziri Macharia afafanua kwa nini chanjo za Korona hazikusafirishwa na Kenya Airways

Waziri wa uchukuzi, James Macharia amesema Shirika la Ndege nchini, Kenya Airways, bado linasubiri ukaguzi wa Shirika la UNICEF ili liruhusiwe kusafirisha chanjo za COVID-19.

Waziri alisema hayo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta alipoandamana na mwenzake wa Afya, Mutahi Kagwe kupokea shehena ya zaidi ya chanjo milioni moja za kukabiliana na maradhi ya COVID-19 za aina ya Oxford-AstraZeneca.

Also Read
Rais wa Tanzania Suluhu Hassan awasili Kenya kwa ziara ya siku mbili

Shehena hiyo iliwasili humu nchini dakika chache kabla usiku wa manane ikiwa kwenye ndege ya Shirika la Ndege nchini Qatar.

Also Read
Barabara ya hewani ya Express Way kufunguliwa siku kuu ya Krismasi mwaka huu

Macharia alisema shirika la Kenya Airways tayari limetia saini mkataba na shirika la UNICEF na linasubiri ukaguzi.

Waziri alisema baada ya kuidhinishwa, shirika hilo litajiunga na mashirika mengine ya ndege ulimwenguni kusafirisha chanjo za maradhi ya COVID-19 Barani Afrika.

Also Read
Kenya na Uganda zazindua matibabu dhidi ya ugonjwa wa Trachoma

Shehena hiyo ya zaidi ya chanjo milioni moja ni sehemu ya kwanza ya dozi milioni zilizotengewa nchi hii.

  

Latest posts

Rais Kenyatta ampokea mwenzake wa Hungary János Áder katika Ikulu ya Nairobi

Tom Mathinji

Majina ya walioteuliwa kwa hazina ya Usawazishaji yachapishwa

Tom Mathinji

Awamu ya pili ya usajili wa wapiga kura yang’oa nanga kote nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi