Waziri Matiang’i kuhojiwa na bunge kuhusu usalama wa Naibu Rais William Ruto

Waziri wa usalama wa kitaifa Dkt. Fred Matiangi Jumatano asubuhi atafika mbele ya kamati ya bunge kuhusu utawala na usalama wa kitaifa huku ajenda kuu ya mkutano huo ikiwa ni usalama wa naibu Rais.

Haya yanajiri baada ya huduma ya taifa ya polisi Alhamisi iliyopita, kufanya mabadiliko katika maafisa wa usalama wanaomlinda naibu rais Dkt. William Ruto kwa kuwaondoa wale wa kikosi cha GSU na kuwapeleka wale wa utawala.

Also Read
Ugonjwa wa kimeta wasababisha vifo vya watu wawili Tanzania

Kupitia kwa taarifa msemaji wa huduma ya taifa ya polisi Bruno Shioso, alisema kuwa kubadilishwa kwa maafisa wa usalama kutoka ulinzi wa majengo ya serikali hadi kwenye makazi ya naibu rais, ni shughuli ya kawaida katika huduma hiyo ili kuimarisha ubora.

Also Read
Viongozi wa kaunti ya Murang'a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Alisema kuwa kitengo cha msafara wa ulinzi wa rais kitaendelea kulinda usalama wa naibu rais. Hatua hiyo iliibua hisia mseto kutoka kwa umma na ulingo wa kisiasa huku wengi wakishutumu hatua hiyo na wengine wakiiunga mkono.

Also Read
Rais Kenyatta kukutana na Maseneta wa Jubilee Jumanne

Runinga ya shirika la utangazaji hapa nchini KBC Channel 1, itapeperusha kikao hicho moja kwa moja.

  

Latest posts

Rais Kenyatta amwomboleza Nancy Karoney, dadake waziri wa ardhi Farida Karoney

Tom Mathinji

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi