Waziri wa Ulinzi apongeza juhudi za wanawake katika kuimarisha usalama humu nchini

Waziri wa ulinzi Monica Juma amewapongeza kina mama kutokana na jitihada zao za kuboresha usalama humu nchini.

Akiwahutubia maafisa wa kike wa jeshi la wana-maji la Kenya, wakati wa kongamano la Athena Jijini Mombasa, Juma alisema jukumu la kuboresha usalama linaboresha uadilifu na pia maarifa ya wanawake.

Also Read
Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Kongamano hilo liliangazia wanawake wataalamu na pia kujiendeleza kwa maafisa binafsi, kujenga mitandao ya usaidizi na kuboresha utenda-kazi.

Kongamano la Athena hujishughulisha na mwongozo kwa wanawake walio katika Wizara ya Ulinzi na pia taasisi nyingine za usalama.

Also Read
Wagonjwa 6 wafariki kutokana na COVID-19 huku watu wengine 1,412 wakiambukizwa

Baadaye, Juma alishiriki kwenye mashindano ya Gofu ya jeshi la wanamaji katika uwanja wa Gofu wa Mombasa, akiandamana na wachezaji wa Gofu kutoka vitengo vyote vitatu vya KDF.

Also Read
Wito watolewa wa kurejeshwa kwa polisi wa akiba Laikipia

Mchezo huo wa Gofu ni semehu ya mipango ya maslahi ya Wizara ya Ulinzi ambayo hudumisha afya ya mwili, baada ya kutambua kwamba afya hiyo inahitajika sana katika utekelezaji wa majukumu ya kijeshi.

  

Latest posts

Kenchic yazindua aina tatu mpya ya bidhaa za kuku

DOtuke

Munya: Covid-19,Nzige na ukame, Chanzo cha gharama ya juu ya maisha

Tom Mathinji

Kenya yaadhimisha wiki ya kimataifa ya kuwanyonyesha watoto

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi