Waziri wa zamani Joseph Nyaga ameaga dunia

Mwansiasa mkongwe na waziri wa zamani Joseph Nyaga ameaga dunia.

Nyaga ambaye alikuwa na umri wa miaka 64 alifariki kutokana na virusi vya Covid-19 katika hospitali moja ya Nairobi akipokea matibabu.

Also Read
Jamii za wafugaji wa kuhamahama watangaza kuunga mkono BBI

Joe Nyaga ni mwanawe Jeremiah Nyagah ambaye alikuwa waziri katika serikali ya hayati mzee Jomo Kenyatta na pia aliyepigania uhuru wa taifa hili.

Joe Nyaga alichaguliwa waziri wa maendeleo ya ushirika katika serikali ya mseto baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Also Read
DCI yawaonya wanafunzi dhidi ya utovu wa nidhamu shuleni

Mwaka 2017 Nyaga alijiuzulu kama mshauri wa Rais Uhuru Kenyatta na kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais kama mwaniaji wa kibinafsi.

Also Read
Himizo la kuunga mkono BBI lashamiri Narok huku ukusanyaji saini ukianza rasmi

Joseph Nyaga alikuwa mwanachama wa kundi la  ‘Pentagon’ la chama cha ODM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Nyaga awali alikuwa mbunge wa Gachoka ambayo sasa ni Mbeere kusini.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi