Wazito FC yawapiga kalamu kocha Kimanzi na wasaidizi wote

Klabu ya Wazito Fc imewatimuwa kocha mkuu Francis Kimanzi ,wasaidizi wake John Kamau  na Jeff Odongo na mkufunzi wa makipa Samuel Okoko.

Hali imekuwa ngumu kifedha kwa klabu hiyo katika siku za hivi punde , huku wachezaji wengi wakitorokea katika vlabu vingine nao wengine kususia mechi ikikisiwa kuwa chanzo kupigwa teke kwa benchi yote ya ukufunzi.

Also Read
Wanajeshi washikwa mateka na wagema Mvinyo Kasarani

Kocha wa timu ya chipukizi Fred Ambani atashika usukani kuwa kocha mkuu,akirejea baada ya kufurushwa miaka miwili iliyopita.

Also Read
Vihiga United waipiga kumbo Kisumu All Stars na kurejea ligi kuu FKF

Wazito Fc waliopoteza  wiki iliyopita dhidi ya  Vihiga Bullets watakuwa nyumbani Jumapili hii kwa pambano la ligi kuu dhidi ya  Nzoia Sugar .

Also Read
Nyamweya aishutumu afisi ya sasa ya FKF kwa matokeo duni ya Harambee Stars

Licha ya kumaliza katika nafasi ya 9 msimu uliopita katika ligi kuu ya FKF kwa alama 45 ,Wazito inakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja,ikiwa na pointi 9 pekee kutokana na mechi 13.

  

Latest posts

Ronaldo kuachiliwa kuondoka Old Traford

Dismas Otuke

Manara na Hersi Matatani

Marion Bosire

Mary Moraa Bingwa wa Mita 800 kwa Wanawake Kwenye Michezo ya Jumuia ya Madola Mwaka 2022

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi