Weasel asusia Kundi jipya la kakake

Mwanzoni mwa juma hili, mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone alianzisha kundi jipya la wanamuziki ambalo alisema lengo kuu ni kutetea maslahi ya wanamuziki wakongwe.

Punde baada ya kubuni “Superstars Association, Jose alichaguliwa kuwa kiongozi na kakake Palasso akachaguliwa kusimamia maswala ya uhusiano mwema.

Hata hivyo kaka yao mwingine ambaye pia ni mwanamuziki kwa jina Weasel hakuhudhuria mkutano wa Jumatatu katika eneo la Kabuusu Jijini Kampala.

Also Read
Kampuni za Nike na MSCHF zaafikiana kuhusu viatu vya shetani

Imebainika kwamba Weasel hakuhusishwa na kaka zake wakubwa kwenye mipango ya kubuni Kundi hilo la wanamuziki ambao wamekuwepo kwa muda mrefu na ndiyo maana hakuhudhuria mkutano ambao ulikuwa na wanamuziki wengine kama vile King Saha na Feffe Bussi.

Weasel alianza muziki akiwa katika Kundi la wawili ambalo lilikuws likiitwa Radio & Weasel na baada ya kifo cha Radio, Weasel alilazimika kuimba peke yake.

Also Read
Will Smith asema yuko tayari kuwania Urais

Haya yanajiri baada ya Chameleone kutetea Kundi lake dhidi ya madai kwamba nia yake ni kung’ang’ania mapato na Kundi la “Uganda Musicians Association (UMA)” ambalo limekuwepo kwa miaka mitatu Sasa.

Also Read
Mechi za Uganda za kufuzu kwa mashindano ya FIBA Afrobasket zaahirishwa kutokana na Covid 19

Jose ana maoni kwamba mahitaji ya wanamuziki wa muda mrefu ni tofauti na yale ya wanamuziki wanaoibukia.

Douglas Mayanja maarufu kama Weasel, Joseph Mayanja maarufu kama Jose Chameleone, Pius Mayanja maarufu kama Pallaso na marehemu Emmanuel Mayanja maarufu kama AK 47 wote ni ndugu na wote ni wanamuziki maarufu nchini Uganda.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi