Wema Sepetu ajitetea

Muigizaji wa filamu za Bongo nchini Tanzania Wema Sepetu amejipata pabaya siku za hivi maajuzi kutokana na hatua yake ya kutangaza biashara za waganga.

Kutangazia watu wengine biashara kumekuwa njia ya kujipatia mapato kwa watu maarufu ambao Wana ufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wema kwa muda wa siku chache zilizopita amekuwa akitangaza biashara nyingi zikiwemo huduma za waganga. Wengi wanahisi kwamba mwanadada huyo amejidunisha mno kwa kutangaza biashara aina hiyo ikitizamiwa ukubwa wa jina lake katika sanaa nchini Tanzania.

Also Read
Eric Omondi apata ubalozi Tanzania

Aristote Kagombe alihojiwa na wanahabari kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Gigy Money ambapo alimkashifu sana Wema kwa kutangazia waganga Biashara. Kulingana naye vitu kama hivyo ndivyo vinamnyima Wema kazi za ubalozi.

Also Read
Bow Wow asherehekea bintiye

Hata hivyo Wema amejitetea akisema yeye hulipisha ada ya juu zaidi kwa matangazo kama hayo jambo ambalo limesababisha wauza bidhaa na huduma kulalamika na ndio maana aliamua kutangaza biashara zote ndogo bila kubagua.

Mtangazaji wa kituo cha redio cha Wasafi Fm Diva amemtetea Wema akisema wanaomkashifu wanaharibu muda wao huku Wema akiendelea kujipatia mapato.

Also Read
Mamito apeleka ucheshi nchini Tanzania

Kulingana na Diva, matangazo hayo humpa Wema zaidi ya shilingi laki mbili za Tanzania kila siku.

Diva anasema kwamba watu wengi maarufu nchini Tanzania ni fukara kiasi cha kukosa chakula kwa sababu ya dhana kwamba hawafai kujihusisha na vitu fulani wakati hivyo vitu vinaweza kuwaletea mapato.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi