Wenyeji Cameroon watinga raundi ya 16 bora AFCON baada ya kuwalabua Ethiopia

Wenyeji Indomitable Lions kutoka Cameroon walijikatia tiketi kwa awamu ra 16 bora ya michuano ya kuwania kombe la AFCON baada ya kuwatitiga  Ethioipia mabao  4-1 katika mechi ya pili ya kundi A iliyosakatwa  katika uchanjaa wa Olembe Alhamisi usiku.

Also Read
Moraa awaangusha vigogo na kufuzu kwa Olimpiki

Nahodha  Vincent Aboubacar  na  Karl Toko Ekambi  walipachika mabao 2 kila mmoja kwa wenyeji ,wakati Dawa Hotessa akifunga goli la pekee kwa Ethiopia maarufu kama Walia.

Also Read
Marekani yaondoa Ethiopia, Mali na Guinea kutoka mpango wa AGOA

Cameroon watarejea uwanjani Jumatatu Januari 17  kwa pambano   la  mwisho  dhidi ya Cape Verde,  wenyeji wakihitaji tu sare ili kuongoza kundi hilo,nao Cape Verde wanawinda sare ili kuingia raundi ya pili  .

Also Read
Afrika yajumuika na China katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi

Katika pambano la pili jingine la mwisho Burkina Faso watakumbana na  Ethiopia ,Burkinabe  wakihitaji pia sare ili kuwa na fursa kufuzu kwa awamu  ya pili.

  

Latest posts

Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Marion Bosire

Didmus Barasa Ajisalimisha kwa Maafisa wa Polisi

Marion Bosire

Chebukati: Tutaharakisha zoezi la kujumlisha matokeo ya kura za Urais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi