Wenyeji Tanzania kufungua dimba la Cecafa Jumapili

Mashindano ya Cecafa  kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Afcon kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka ujao nchini Mauritania yataanza kutimua vumbi Jumapili hii mjini Arusha Tanzania huku mataifa 9 yaliyotengwa katika makundi matatu ya timu tatu kila moja  yakiwinda tiketi hizo mbili za Afcon.

Also Read
Mtoto Noman apata kazi ya ubalozi

Mabingwa watetezi na wenyeji Tanzania almaarufu Ngorongoro Heroes watashuka  uwanjani Black Rhino Academy kuanzia saa kumi alasiri siku ya Jumapili Novemba 22 kwa pambano la ufunguzi la kundi A dhidi ya Djibouti.

Wachezaji wa Ngorongoro Heroes ya Tanzania  wakiwa mazoezini

Sudan kusini itafungua ratiba ya kundi B Jumatatu dhidi ya Uganda wakati Kenya pia ikimenyana na Ethiopia katika mchuano wa Kundi B pia jumatatu.

Also Read
Mkanda uliotupwa na Ronaldo wasaidia kuchangisha shilingi milioni 8 kumtibu mtoto mmoja Serbia

Mechi za makundi zitakamilika Ijumaa  hii Novemba 27 ambapo timu bora kutoka kila kundi na timu ya pili bora kutoka makundi yote matatu zikicheza  nusu fainali  Novemba 30 ikifuatwa na fainali ya Desemba 2.

Also Read
Prof Tom Ojienda asema kesi za uchaguzi wa Fkf hazina msingi
Tanzania wakipiga fainali ya mwaka jana dhidi ya Kenya

Timu mbili bora zitafuzu kwa michuano ya Afcon ya Januari na Februari mwaka ujao  nchini Mauritania.

Tanzania waliishidna Kenya bao moja kwa bila katika fainali ya mwaka uliopita nchini Uganda.

  

Latest posts

Tusker kushikana mashati na Gor Mahia mechi ya kufungua pazia la msimu kuwania kombe la supa

Dismas Otuke

Isabella Mwampambo mkuzaji vipaji vya soka Upendo Friends Sports Academy mjini Arusha Tanzania

Dismas Otuke

Shujaa yashindwa fainali ya kombe kuu na Afrika Kusini 5-38 Vancouver 7’s

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi