WHO: Afrika inahitaji dozi milioni 20 za dawa ya Astrazeneca

Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa shirika la afya duniani –(WHO) Dkt. Matshidiso Moeti, alisema bara hili linahitaji angalau dozi million 20 za dawa ya chanjo ya AstraZeneca kufikia kati kati ya mwezi Julai, ili kuhakikisha kwamba wale waliopewa chanjo ya kwanza wanachanjwa tena kwa wakati ufaao.

Also Read
Wizara ya Afya yaripoti visa vipya 1,065 vya Corona

Dkt. Moeti alisema kupitia kitandaazi cha tweeter kwamba bara la Afrika linahitaji chanjo kwa sasa, huku akionya kwamba hatua zozote za kusitisha kampeini ya chanjo itamaanisha kupotea kwa maisha na pia matumaini.

Pia alisema kwamba dozi milioni – 200 zaidi zinahitajika ili kuhakikisha kwamba bara la Afrika linatoa chanjo kwa asilimia 10 ya wakaazi wake kufikia Septemba mwaka huu.

Also Read
Kenya yaanza kutoa awamu ya pili ya chanjo ya Astrazeneca

Dkt. Moeti alihimiza mataifa ya bara hili ambayo tayari yamewapatia chanjo raia wao walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa corona yakubali kusambaza dozi zao ili kuhakikisha kwamba kila mmoja anapa kinga dhidi ya Covid 19.

Also Read
Mataifa 9 Barani Afrika yaharibu dozi elfu 450 za AstraZeneca

Kufikia tarehe 26 mwezi Mei, bara la Afrika lilikuwa limenakili zaidi ya visa million 4.7 vya ugonjwa wa corona na karibu vifo vya watu elfu- 130 kutokana na ugonwja huo.

  

Latest posts

Kenya imenakili visa 26 vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Rais Kenyatta: Mataifa ya Afrika Sharti yakabiliane kikamilifu na zimwi la Ufisadi

Tom Mathinji

Watu wawili wafariki baada ya jengo kuporomoka Kiambu

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi